Filamu

Wakala afichua chanzo cha kifo cha Sam Neill

AUSTRALIA: Muigizaji nguli wa Hollywood aliyepata umaarufu mkubwa kupitia filamu ya ‘Jurassic Park’, Sam Neill, amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 78.

Licha ya taarifa iliyotolewa na familia yake ikieleza kuwa Neill alifariki Julai 13, 2026 mjini Sydney, Australia, akiwa amezungukwa na familia yake. Wakala wake wa muda mrefu Philip Grenz amefafanua kuwa chanzo cha kifo hicho kilikuwa ni ugonjwa wa nimonia.

Grenz ameibuka baada ya kusambaa kwa taarifa zisizo sahihi kuhusu kifo cha muigizaji huyo. Grenz amebainisha kuwa kabla ya kuugua nimonia, Neill alikuwa amefanikiwa kuishinda saratani ya damu aina ya ‘angioimmunoblastic T-cell lymphoma’ kupitia matibabu ya kisasa ya CAR-T, na alitangazwa kutokuwa na saratani.

Grenz aliendelea kueleza kuwa licha ya changamoto za afya alizopitia katika miaka ya karibuni, Sam Neill aliendelea kuwa na shughuli nyingi za kisanii. Kwa mujibu wa wakala wake, alikamilisha miradi minne ya filamu ndani ya mwaka mmoja.

Familia yake imeeleza kuwa itafanya ibada ya faragha ya kumuaga kwenye shamba lake nchini New Zealand, huku wakisisitiza kwamba hakutakuwa na shughuli kubwa kwa kuwa mwenyewe kutopenda shughuli kubwa za hadhara.

Sam Neill atakumbukwa kama mmoja wa waigizaji mashuhuri zaidi duniani, akiwa ameacha alama kupitia filamu kama ‘Jurassic Park’, ‘The Piano’, ‘The Hunt for’ Red October’, ‘Dead Calm’ na ‘Jurassic World Dominion’.
Tangu kutangazwa kwa kifo chake, viongozi wa tasnia ya filamu, waigizaji na mashabiki kutoka mataifa mbalimbali wameendelea kutoa salamu za rambirambi, wakimsifu kwa kipaji chake, unyenyekevu na mchango mkubwa alioutoa katika historia ya sinema duniani.

Related Articles

Back to top button