Wekezeni kwenye walimu-Mwakinyo

BONDIA wa Tanzania, Hassan Mwakinyo amewashauri mabondia nchini kuwekeza kwa walimu wazuri wa ngumi, kwani mchezo huo unaingiza pesa nyingi.
“Ngumi ni pesa, ngumi ni maisha na sio usela tena kama ilivyozoeleka. Hii ni fursa tafuteni walimu wa ngumi wazuri wenye weledi wa kweli”.
Mwakinyo ameandika kwenye ukurasa wake wa istagramu ‘’Jana nilipokea simu ya shabiki mmoja mwenye hekma sana na mahaba juu ya mchezo wa ngumi akanieleza yakua boxing’s is dangerous sport in the world!! you have to be verry carefull”
‘’Serikali kwa maana ya wizara na vyombo vya habari vya Tanzania na baadhi ya na kampuni na watu binafsi wana jitahidi sana kuonyesha kusupport mchezo wetu Alhamdulilah na mimi nasema kua Ngumi ni pesa ngumi ni maisha na sio usela tena kama ilivyo zoeleka.’’
‘’Hii ni fursa tafuteni walimu wa ngumi wazuri wenye weledi wa kweli achaneni na waganga kua mganga mzuri sio kua mwalimu mzuri wa boxing elimu ya boxing sio ya uganga na ramli Colorada King bendera puto mlingoti sindano sukudu’’ameandika Mwakinyo




