Masumbwi

Serikali yawapiga msasa mabondia

DAR ES SALAAM: SERIKALI imewataka mabondia wa ngumi za kulipwa kuwa makini na mikataba wanaosaini wanapopanda ulingoni kucheza mapambano ya kitaifa na kimataifa.

Mwenyekiti wa Baraza la Michezo la Michezo la Taifa (BMT), Leodegar Tenga ambaye ni mgeni rasmi katika semina ya mabondia iliyoandaliwa na TPBRC kwa kushirikiana na BMT iliyofanyika Ilala, amesema mchezo wa ngumi umeiletea heshima taifa, kushika nafasi ya pili kwa kupendwa nchini.

“Mabondia mnapaswa kuwa makini na kutambua vipengele vya mkataba mnayoingia kwenda kupigana iwe Tanzania au nje ya nchi bila kuangalia zaidi kiasi cha fedha.

Mara nyingi wanaangalia zaidi kiasi cha fedha kuliko kuangalia vipengele vya mikataba wanayoingia kwa sababu baadhi yao wananyonywa na kukosa haki zao za msingi,” amesema.

Tenga amesema mbali n mikataba pia mabondia wanatakiwa kujitangaza kupitia mchezo huo na kuweza kupata wadhamini na kujiongezea kipato.

“Kuna suala la Afya, mabondia wanatakiwa kujitunza kweli katika maisha ya kawaida wawe waangalifu na matumizi ya Mjani (Bangi) na kutumia dawa haramu za kusisimua mwili zinazokatazwa michezo,” amesema.

Naye Katibu Mtendaji wa BMT, Neema Msitha amewaasa mabondia kutumia ushawishi wao kujitangaza zaidi kupitia mitandao ya kijamii ili waweze kujipatia kipato nje ya mapambano .

“Mchezo wa ngumi kwa sasa unafuatiliwa sana tumieni mitandao ya kijamii kujitangaza kupata soko kwa sababu ukishinda Knockout watu watakufahamu baada ya hapo hakuna atayekufuatilia,” amesema.

Akizungumzia suala la mikataba, Msitha amesema mabondia wanatakiwa kuwa makini katika mafunzo hayo kwa sababu wanapokea malalamiko mengi kuhusu mikataba wanayoingia na mapromota.

“Mikataba wanayoingia mabondia wanatakiwa kuelewa kuepuka kudhulumiwa ndani ya ngumi kuna ujanja ujanja mwingi, promota hutumia madhaifu ya mabondia kutoelewa vipengele vya mkataba kuwadhulumu fedha,” amesema Msitha.

Related Articles

Back to top button