Vunjabei ampa Rais Samia Mkanda wa WBF
DAR ES SALAAM: BONDIA wa ngumi za kulipwa nchini, Halima Vunjabei ametoa zawadi ya mkanda wake wa ubingwa Dunia wa WBF International kwa Rais Samia Hassan baada ya kumchakaza mpinzani wake Songuel Ayten raia wa Uturuki kwa Knockout ya raundi ta tatu nchini Ujerumani.
Vunjabei amekabidhi mkanda huo leo mchana kwa Katibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Sanaa Utamaduni na Michezo, Gerson Msigwa wakati alipokuwa akimakabidhi zzawadi ya Sh milioni tano ya Knockout ya Mama.
Wikiendi iliopita, Vunjabei aliweka rekodi mpya nchini katika mchezo wa ngumi za kulipwa ya kuwa mwanamke wa kwanza kushinda mkanda wa ubingwa nje ya nchi katika pambano ambalo limefanyika nchini Ujerumani.
Akizungumza mara baada ya kutoa zawadi hiyo, Msigwa alimpongeza bondia huyo kwa kuitangaza nchi pamoja na kushinda mkanda huo huku akimtaka kuendelea kuwatwanga wengine katika mapambano ya kimataifa.
“Hongera Halima kwa kuipeperusha vyema bendera ya Tanzania nje pamoja na ushindi wa mkanda wa kimataifa wa WBF ulioshinda nchini Ujerumani lakini nataka uendelee kupiga hatua nyingine ya kuleta mikanda zaidi, nampa hii shilingi milioni tano ya Knockout ya Mama kutokana na kile ambacho akifanya Ujerumani,” amesema.
Lakini kwa upande wa Vunjabei ameishukuru BMT na Rais Samia Suluhu Hassan kwa zawadi ya shilingi milioni tano ya Knockout ya Mama huku akiomba mkanda wake alioshinda Ujerumani apelekewe Rais Samia.
“Naishukuru BMT, Kamisheni ya ngumi za kulipwa nchini na serikali kupitia Rais Samia kwa sapoti kubwa ambayo wanatupa, sina chakumlipa Mama lakini mkanda huu wa ubingwa naomba afikishiwe kama zawadi yangu kwake.