
DAR ES SALAAM: MSANII wa Vichekeshaji na mtoto wa msanii Anko Zumo, maarufu kwa jina la Mai Zumo, amehitimu rasmi elimu ya msingi baada ya kumaliza Darasa la Saba, hatua muhimu inayomfungulia ukurasa mpya katika safari yake ya masomo.
Mai Zumo, ambaye amejizolea umaarufu kupitia vichekesho na vipaji vyake mbalimbali tangu akiwa mdogo, sasa anajiandaa kuanza elimu ya sekondari huku akimuomba Mungu amuongoze na kumlinda katika hatua hiyo mpya ya maisha.

Kupitia ujumbe wake, Mai Zumo ameonesha shukrani kwa Mungu, wazazi na walimu kwa kufanikisha safari yake ya elimu ya msingi na kueleza matumaini makubwa aliyonayo kuelekea masomo ya sekondari.
Mahafali yake yamepokelewa kwa furaha na pongezi kutoka kwa mashabiki, ndugu, jamaa na wadau mbalimbali ambao wamekuwa wakifuatilia ukuaji wake katika tasnia ya burudani pamoja na masomo.
Wengi wamepongeza juhudi zake za kuweza kuendelea vizuri na elimu sambamba na vipaji vyake vya sanaa, wakimtaka kuendelea kuwa mfano bora kwa watoto na vijana wengine.
Pongezi pia zimeelekezwa kwa familia ya Anko Zumo kwa malezi na usimamizi mzuri uliomwezesha Mai Zumo kufikia hatua hiyo muhimu ya elimu.
Kwa sasa, Mai Zumo anatarajia kuanza safari mpya ya elimu ya sekondari akiwa na ndoto na matumaini ya kufanya vizuri zaidi katika masomo na kukuza vipaji vyake.
Hongera Mai Zumo kwa kuhitimu Darasa la Saba. Tunakutakia kila la heri na mafanikio makubwa katika hatua inayofuata ya elimu na maisha yako.




