Familia

Zari alia na wanaotoa mimba

MFANYABIASHARA Zarina Hassan maarufu Zari the boss lady ameandika ujumbe wa kumpongeza mtoto wake wa kwanza, Pinto baada ya kutimiza miaka 21 tangu kuzaliwa kwake huku akiwaponda wanawake wanaotoa mimba.

 

Mama huyo aliyejawa na furaha alitumia mitandao ya kijamii kusambaza picha zake tangu kuzaliwa hadi sasa.

 

Katika ujumbe wake, Zari amesisitiza umuhimu wa kuwatunza mtoto, akitafakari uamuzi wake wa kujifungua. Pia amewaonya wasichana dhidi ya utoaji mimba, akipendekeza kwamba alifanya chaguo sahihi kujifungua.

 

“Wasichana, huyo mwanaume ambaye unatoa mimba zake naye ana wanawake watano wengine wanaofanya hivyo hivyo, mwisho wa siku uantamani utulie na uwe na watoto, unajikuta haiwezekani.

 

Tumia kinga au uwe na mtoto wako”, ameandika Zari kwenye ukurasa wake wa Instagram.

 

.

Back to top button