Familia

‘Timizeni ahadi zenu kwa mtoto wa marehemu Fredy’

DAR ES SALAAM: NAIBU Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Hamisi Mwinjuma ‘Mwana FA’ amewataka watu wote waliotoa ahadi za kuchangia ada ya mtoto wa marehemu, Fredy Kiluswa kuhakikisha wanalitimiza hilo na wizara itakuwa ikifuatilia.

Mwana FA ametoa salamu hizo katika ibada ya kuaga mwili msanii huyo aliyefariki mnamo Novemba 16, 2024 katika Hospitali ya Mloganzila Jijini Dar es Salaam.

” Wizara pamoja na Taasisi zake imetoa mkono wa rambirambi kwa familia na ninaomba fedha hizo ziwe kwa ajili ya familia na kuhusu gharama nyinginezo za msiba ambazo zitakuwa bado hazijakamilika ninaomba mzikamilishe wenyewe bila kuisumbua familia,”

Baadhi ya wadau waliotoa ahadi za kumsomesha mtoto wa marehemu ni Mwenyekiti wa Mama Ongea na Mwanao Steve Mengele maarufu kama Steve Nyerere ambapo alisema atalipa Ada ya Mwaka mmoja na Msambazaji wa kazi za Sanaa Alex Msama alisema atalipa Ada ya miaka mitatu.

Naye Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Sanaa kutoka Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Dk Emmanuel Ishengoma aliwapongeza wadau wa tasnia ya filamu kwa umoja wao na kusisitiza wasanii kuishi maisha ya kuacha alama nzuri kwenye jamii kama ilivyokuwa kwa marehemu Fredy Kiluswa.

Back to top button