Duwaa atema madini!

DAR ES SALAAM: MSANII na Mtengeneza maudhui anayefanya vizuri kwa sasa, Abigael Duwaa, amewakumbusha wanajamii umuhimu wa kuwatunza wazazi wao wakiwa bado hai, akisisitiza kuwa fursa hiyo ni ya kipekee na haijirudii.
Kupitia ukurasa wake wa mitandao ya kijamii, Abigael ameandika ujumbe wenye kugusa hisia za wengi akisema:
“Tutunze wazazi wetu pindi wanapokuwa hai, maana akienda ameenda, huwezi pata kama yeye.”
Kauli hiyo imeibua tafakari kwa wengi, ikikumbusha thamani ya wazazi katika maisha ya kila mtu. Ujumbe wa Abigael unaonesha wazi kuwa wazazi ni nguzo muhimu katika familia na jamii kwa ujumla, na wanastahili upendo, heshima na matunzo wakati wote.
Katika jamii ya sasa, kumekuwa na changamoto ambapo baadhi ya watoto hushindwa kuwajali wazazi wao, hasa wanapofanikiwa kimaisha.
Wapo wanaochagua kuwatenga wazazi wao na kutanguliza mahusiano au malezi ya watu wengine, jambo ambalo si sahihi na halina busara.
Ujumbe wa Abigael Duwaa unatoa somo muhimu kuwa mafanikio hayana maana kama hatuwakumbuki na kuwathamini wale waliotulea na kutusimamia tangu utotoni.
Ni wajibu wa kila mmoja kuhakikisha wazazi wanapata faraja, upendo na heshima wanayostahili wakiwa bado nasi.




