Rakeem wa Jux atimiza miezi sita, amchagua baba yake

DAR ES SALAAM: MSANII wa Bongo Fleva, Juma Mkambala (Jux), pamoja na mke wake Priscilla, wanasherehekea kutimia kwa miezi sita tangu kuzaliwa kwa mtoto wao, Rakeem.
Kupitia kurasa zao za Instagram, familia hiyo imechapisha video inayoonesha tukio la furaha wakiwa pamoja na mtoto wao.
Katika video hiyo, Rakeem anaonekana akicheza mchezo wa kuchagua kati ya upande wa Baba na Mama, ambapo hatimaye alimchagua Baba, jambo lililozua furaha na vicheko kwa wazazi hao.

Sambamba na video hiyo, waliandika ujumbe wenye hisia ukisema:
“Alhamdulillah, kwa mtoto huyu mdogo aliyetuibia mioyo yetu, Rakeem heri ya nusu mwaka nyota mdogo! Miezi 6 ya kung’ara kwa nguvu na kutuletea furaha kubwa. Tunakupenda zaidi kuliko hapo awali na tutafanya lolote kuhakikisha unafurahia siku zote.”
Rakeem alizaliwa Agosti 24, 2025, na tangu wakati huo amekuwa chanzo cha furaha kubwa kwa familia hiyo na mashabiki wao kwa ujumla.
Sherehe hiyo ya miezi sita imeonesha upendo na mshikamano mkubwa ndani ya familia hiyo maarufu kwenye tasnia ya burudani nchini.




