Mastaa

Wolper: Alikiba ndiye penzi langu la kwanza

....napenda wimbo wake ‘Mapenzi yana run dunia’

DAR ES SALAAM: Msanii wa filamu nchini, Jacqueline Wolper, amefunguka kuwa bado ni shabiki mkubwa wa mwanamuziki wa Bongo Fleva, Alikiba, huku akitaja wimbo wake ‘mapenzi yana run dunia’ kuwa ndio wimbo anaoupenda zaidi.

Akizungumza hivi karibuni, Wolper amesema licha ya miaka kupita tangu walipowahi kuwa kwenye mahusiano, bado anamkubali Alikiba kama msanii mwenye kipaji na mwenye mapenzi ya dhati.

Ameeleza kuwa Alikiba alikuwa mpenzi wake wa kwanza na akamsifu kwa sifa zake nzuri, akimtaja kuwa ni mtu mwenye upendo.

“Mimi ni shabiki wake. naupenda sana wimbo wake Mapenzi Yana Run Dunia. Pia naamini msemo unaosema usitupe Big G kwa sababu ya kuonjeshwa karanga,” amesema Wolper.

Kauli hiyo ya Jacqueline imeibua maneno miongoni mwa mashabiki, huku wengi wakikumbuka historia ya mahusiano yaliyowahi kuwahusisha Wolper na Alikiba miaka iliyopita.

Related Articles

Back to top button