Muziki

DAVIDO: “B4 B4” yaendelea kushika namba moja kwa wiki ya nne Nigeria

LAGOS: Wimbo wa ‘B4 B4’ wa staa wa muziki wa Nigeria, David Adeleke maarufu Davido, alioshirikiana na wasanii Mayorkun na FOLA, umeendelea kufanya vizuri kwenye chati ya muziki nchini Nigeria baada ya kushika nafasi ya kwanza kwa wiki nne mfululizo.

Kwa mujibu wa Official Nigeria Top 100, ‘B4 B4’ imeendelea kuwa wimbo unaoongoza chati hiyo, huku ukibaki katika nafasi ya kwanza kwa wiki ya nne tangu ulipoingia kwenye chati.

Mafanikio hayo yanaongeza rekodi ya Davido katika soko la muziki la Nigeria, huku ushirikiano wake na Mayorkun pamoja na FOLA ukiendelea kuvuta usikivu wa mashabiki wa muziki wa Afrobeats.

Katika orodha hiyo, ‘Heaven Baby’ ya Ayra Starr akimshirikisha ZAYN imeshika nafasi ya pili, wakati “GTA” ya Seyi Vibez ikiwa nafasi ya tatu.

Wachambuzi wa masuala ya Muziki nchini Nigeria wamesema huenda Davido akaendelea kuongoza katika chati hiyo kutokana na wimbo huo kuonekana kupendwa zaidi nchini humo kwa sasa.

Related Articles

Back to top button