Kajala amshukuru Lamatah kwa kumzawadia kiwanja

DAR ES SALAAM: MSANII wa filamu nchini Tanzania, Frida Kajala Masanja, amemtumia shukrani za dhati rafiki yake Lamatah kupitia ukurasa wake wa Instagram baada ya kumpatia zawadi ya kiwanja katika maadhimisho ya siku yake ya kuzaliwa.
Kajala amesema zawadi hiyo imegusa moyo wake kwa kiasi kikubwa na kuonyesha upendo, ukarimu na kujali alionao Lamatah.
Ameeleza kuwa rafiki huyo si tu rafiki wa kawaida, bali amekuwa sehemu ya familia yake.
Katika sehemu ya ujumbe wake, Kajala ameandika:
“My dearest best friend, Kuna watu Mungu huwaleta kwenye maisha yetu kama marafiki, lakini mwisho wake wanakuwa familia.
Wewe ni mmoja wao. Asante kwa kuniongezea asset nyingine. Ulichonifanyia jana kimenigusa kwa namna ambayo siwezi kuelezea kwa maneno.
Kuninunulia kiwanja ni zawadi ambayo si kila mtu anaweza kutoa, na imenionyesha jinsi ulivyo na moyo wa upendo, ukarimu, na kujali. Nakupenda sana, Mungu akutunze kwa ajili yangu, Lamatah.”
Ujumbe huo umevutia hisia za mashabiki wengi, ambao wamempongeza Lamatah kwa zawadi hiyo ya kipekee na kumtakia Kajala heri na mafanikio zaidi katika maisha yake.




