Nyota ya Dolly yaharibiwa

CALIFORNIA: TAARIFA mpya ni kuwa nyota ya hayati Dolly Parton iliyopo eneo la Hollywood Walk of Fame imeharibiwa na maua yaliyowekwa awali kuibiwa.
Taarifa zaidi kutoka Mtandao wa Complex zimefafanua kuwa tukio hilo limefanywa na baadhi ya mashabiki na haijafahamika ni kwa sababu gani.
Imeripotiwa kuwa siku chache tangu kutangazwa kifo cha nguli huyo wa muziki wa Country, mashabiki walimiminika katika nyota hiyo na kuweka maua, mishumaa na jumbe mbalimbali za kumuenzi lakini sasa vimeibiwa na nyota hiyo kuchorwachorwa na kusilibwa.
Aidha, licha ya kupokea taarifa hizo lakini Hollywood Chamber of Commerce, ilisema inafahamu juu ya nyufa zilizokuwepo awali katika nyota hiyo na walishapanga kufanya ukarabati wiki hii.
Dolly alitunukiwa nyota kwenye Hollywood Walk of Fame mnamo Juni 14, 1984 na alifariki Agosti 25, mwaka huu akiwa na umri wa miaka 80.
Alifariki Nashville, Tennessee akiwa amezungukwa na familia yake iliyothibitisha kuwa mpendwa wao huyo alifariki kwa kansa.




