Nyumbani

Michuano ya wanawake U17 Cecafa kuanza Juni 13

DAR ES SALAAM: MICHUANO ya Soka la Wanawake kwa vijana chini ya umri wa miaka 17 ya Afrika Mashariki na Kati inayoandaliwa na Baraza la Vyama vya Soka ukanda huo (Cecafa) imepangwa kufanyika Dar es Salaam kuanzia Juni 13 hadi 23, 2026.

Kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa jana, Tanzania, Kenya, Sudan na Somalia zipo Kundi A, huku Uganda, Djibouti, South Sudan na Zanzibar zikiwa Kundi B.

Tanzania itafungua dimba na Somalia katika mchezo utakaochezwa kwenye Uwanja wa KMC Dar es Salaam Juni 13, baadaye itacheza na Sudan na kuhitimisha dhidi ya Kenya.

Mashindano haya ni jukwaa muhimu la kukuza vipaji vya wasichana, kujenga uzoefu wa kimataifa na kuandaa nyota wa baadaye wa soka la wanawake.

Kikosi cha Serengeti Girls kiko kambini kikijiandaa na mchezo wa kufuzu Kombe la Dunia dhidi ya Afrika Kusini. Mchezo huo utaendelea kukiimarisha na kuwa tayari kwa michuano ya Cecafa.
Mwisho

Related Articles

Back to top button