Ligi KuuNyumbani

Yanga yatibua rekodi ya kadi

Kadi nyekundu aliyooneshwa winga wa Yanga Jesus Moloko katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Mbeya city leo imekuwa ya kwanza kwa klabu hiyo msimu huu.

Moloko ameoneshwa kadi hiyo pamoja na mchezaji wa Mbeya City Hassan Nassoro baada ya kufanyiana vitendo visivyo vya kiungwana wakati wa mchezo huo kwenye uwanja wa Sokoine jijini Mbeya.

Hadi mapumziko Yanga ilikuwa nyuma kwa mabao 2-0 na hadi mwisho wa mchezo timu hizo zimetoshana nguvu kwa sare ya mabao 3-3.

Itawapasa Mbeya City kushinda michezo miwili ya mtoani ili kusalia ligi kuu

Matokeo michezo ya ligi hiyo ambayo tayari imemalizika leo ni kama ifuatavyo:

Mbeya City 3 – 3 Yanga
Singida BS 2 – 1 Ruvu Shooting
Tanzania Prisons 1 – 0 KMC
Mtibwa Sugar 3 – 0 Kagera Sugar
Ihefu 3 – 1 Geita Gold
Coastal Union 0 – 2 Azam

Related Articles

Back to top button