Ligi Kuu

Coastal haitacheza kinyonge dhidi ya Yanga

DAR ES SALAAM: COASTAL Union imewataka mabingwa watetezi Yanga kutarajia upinzani mkali watakapokutana katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara kesho, huku Kocha wa Coastal Union, Fikiri Elias akisisitiza kuwa timu yake haitacheza kwa woga.

Fikiri amesema kikosi chake kimeutumia vizuri muda wa maandalizi kwa kufanya maboresho muhimu ndani ya siku mbili zilizopita ili kuhakikisha kinakuwa tayari kwa mchezo huo mgumu dhidi ya Yanga.

“Sisi kama Coastal Union tumejiandaa vizuri kabisa, tumepata nafasi ya kufanya maboresho na kuandaa mbinu zetu kuelekea mchezo huu huku tukifahamu ubora wa Yanga,” amesema Fikiri.

Kocha huyo amesema wanafahamu Yanga wanapambana kuhakikisha wanatwaa ubingwa kwa mara nyingine, lakini Coastal Union nayo ina malengo yake ya kumaliza ligi katika nafasi nzuri.

“Yanga watakuja kuuliza maswali na Coastal tutakuwa tayari kuyajibu. Tunategemea mchezo mzuri wenye ushindani mkubwa,” amesema.

Fikiri ameongeza kuwa wachezaji wake wana morali kubwa kuelekea mchezo huo na wako tayari kupambana kuhakikisha wanapata matokeo chanya mbele ya vigogo hao wa Dar es Salaam.

Related Articles

Back to top button