Ligi Kuu

Mrithi wa Gamondi Yanga anatisha

DAR ES SALAAM:KLABU ya Yanga imetangaza kuachana na kocha Miguel Gamondi. Taarifa ya Yanga iliyotolewa leo imeeleza kuwa imeachana pia na kocha msaidizi Mussa Ndaw.

Gamondi amedumu Yanga kwa mwaka mmoja na nusu na sasa Yanga wameona imetosha. akiwa Yanga kocha huyo ameipa ubingwa wa ligi, kombe la shirikisho pamoja na kuifikisha Yanga robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Yanga wameutaarifu umma kuwa tayari mchakato wa kocha mpya umeanza na umefikia pazuri.

Hata hivyo taarifa ambazo SpotiLeo inazo ni kuwa tayari kocha anayetarajiwa kuvaa viatu vya Gamondi amewasili nchini na muda wowote atatambulishwa.

 

 

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button