Ligi Kuu

‘Mtibwa Sugar lazima ipambane’

DAR ES SALAAM: KOCHA wa Mtibwa Sugar FC, Yusuph Chipo amesema timu yake inapaswa kujipanga upya haraka kuelekea mchezo ujao dhidi ya Singida Black Stars baada ya kuendelea kupata matokeo mabaya kwenye ligi.

Mtibwa Sugar imetoka kupoteza mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya Dodoma Jiji kwa kichapo cha bao 1-0 jana.

Chipo amesema kupoteza mchezo wa tatu mfululizo kunaiweka Mtibwa Sugar kwenye mazingira magumu zaidi katika msimamo wa ligi, huku akisisitiza umuhimu wa timu hiyo kupambana ili kujinusuru na hatari ya kushuka daraja.

“Tunarudi kujipanga kujiandaa na mchezo ujao dhidi ya Singida Black Stars. Kuendelea kupoteza mchezo wa tatu mfululizo kunatuweka mahali pabaya zaidi,” amesema Chipo.

Amesema suluhisho kubwa kwa sasa ni kuhakikisha timu inaanza kutumia vizuri nafasi za kufunga mabao ili kujiondoa kwenye eneo hatari la msimamo.

“Siri ni kupambana kufunga mabao na kutoka tulipo ili tusije kushuka daraja,” amesema.

 

Related Articles

Back to top button