La Liga
Zubimendi aigomea Liverpool
KIUNGO wa Real Sociedad, Martin Zubimendi amekataa ofa ya kujiunga na Liverpool, hivyo Mhispania huyo ameamua kubali Reale Arena.
Zubimendi ,25, aliyeisaidia Hispania kushinda Euro 2024, alikuwa akiwindwa na Liverpool baada ya kuambiwa huenda akaondoka Sociedad.
Kwa mujibu wa mwandishi wa habari za michezo kutoka nchini Italia, Fabrizio Romano, Real Sociedad ina mpango wa kumuongezea mkataba kiungo huyo. Zubimendi awali alikataa ofa ya kujiunga Arsenal na Bayern Munchen.
Zubimendi alijiunga na Sociedad akitokea timu ya vijana Sociedad C,mwaka 2016, baada ya hapo alijiunga na Sociedad B mwaka 2018 kisha timu ya kubwa mwaka 2019.