Ndoto ya Hitler inayotimizwa na Mbappe
Miaka 135 iliyopita kule Austria-Hungary alizaliwa mwanadamu aliyeigeuza dunia chini juu juu chini ili kutimiza ndoto zake
Baada ya kupigana vita ya kwanza ya dunia 1919 kama mwanajeshi wa Ujerumani miaka miwili baadae alichaguliwa kuwa kiongozi wa chama cha Nazi hapo harakati zake za kuitawala dunia zikaanza
Historia inamtambua Adolf Hitler kiongozi wa chama cha Nazi kama moja ya chanzo cha vita ya pili ya dunia baada ya kugeuka dikteta na kuivamia Poland yote ikiwa ni kutimiza ndoto yake
Ndoto ya Hitler ilileta uharibifu vifo umasikini utumwa ila hakujali alikuwa tayari kwa lolote ilimradi itimie
Hitler alifariki kwa kujipiga risasi April 30 1945 alipofahamu ndoto yake ya kutawala dunia haitotimia baada ya kuwekwa wazi Ujerumani itapoteza vita hiyo
Miaka 53 baadae pale Paris, Ufaransa alizaliwa kijana aliyebeba ndoto ya Hitler ila haikuwa kuitawala dunia kisiasa wala kiuchumi bali ni kupitia Soka akiamini huku atatimiza pale alipofeli Hitler
Alianza harakati zake kaskazini mashariki mwa Jiji la Paris akikipiga AS Bondy chama lake la mtaa hadi alipofikisha miaka 14 akahama jiji kujiunga na timu ya vijana pale Monaco
2015 alipandishwa timu ya wakubwa ndipo akawa mwanajeshi na kuanza kupigana vita akavunja rekodi ya kuwa mchezaji mdogo zaidi kuwahi kuitumikia Monaco akimpiku Thierry Henry akaisaidia Monaco kubeba taji la Ligue 1 na kufika robo fainali ligi ya mabingwa barani ulaya
Tetesi zikafika Bondy kuhusu mabalaa ya kijana wao kule Monaco na stori kuhusu uwezo wake zikasambaa jiji zima la Paris kama propaganda za kinazi mabwanyenye wa Paris wakazisikia
August 2017 PSG walimsaini Mbappe kwa mkopo kutoka Monaco kukiwa na kipengele cha kumnunua kwa €180M na kukamalisha usajili huo mwaka mmoja baadae
2018 Mbappe alishinda taji la dunia akiwa na Ufaransa ndipo ulimwengu ukamvika ufalme
Pale Ligue 1 Mbappe amebeba kila kombe pia tuzo zote binafsi akiifungia PSG magoli 255 kwenye michezo 305 akiwa mfungaji bora wa muda wote pale Paris
Juni 3 2024 Real Madrid wanakamilisha usajili wa Kylian Mbappe kama mchezaji huru kutoka PSG
Tofauti na Hitler Mbappe amenukuliwa akikiri kutimiza ndoto zake baada ya kujiunga na Real Madrid