Mastaa

Zawadi ya Lamborghini yamstua Diana Bahati

NAIROBI: MWANAMUZIKI na mfanyabiashara Bahati amedokeza kwamba zawadi itakayofuata kumnunulia mke wake, Diana, itakuwa ni gari aina ya Lamborghini kauli iliyoibua mijadala kwa Wakenya katika mitandao ya kijamii.

Licha ya kumzawadia zawadi mbalimbali zenye thamani kubwa mke wake, Diana Marua ameweka picha ya gari alilozawadiwa na mume wake huyo aina ya Brabus G-Wagon gari ambalo limekuwa maarufu mno kwenye mitandao ya kijamii nchini Kenya huku akisema.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Diana alishiriki picha yake akiwa na gari hilo la kifahari, akinukuu: “Diana Brabus, nitakuwa muongo kama nitasema maisha sio mazuri.”

Bahati ambaye ni mumewe akamjibu: “Gari hili limetengeneza vichwa vya habari vingi na zawadi inayofuata itakuwa Lamborghini.”

Ikumbukwe kuwa mwezi Februari, Bahati aligonga vichwa vya habari baada ya kumshangaza mkewe Diana na gari aina ya Brabus yenye thamani ya fedha za Kenya milioni 45.

Ilikuwa zawadi ya nane na ya mwisho katika mfululizo wa kuashiria safari yao ya miaka nane pamoja na maisha yao yenye watoto watatu.

Hali hiyo ilimtoa machozi ya hisia Diana wakati alipokuwa akikabidhiwa gari hilo lililokuwa mfululizo wa zawadi kutoka kwa mume wake mwanamuziki na mfanyabiashara Bahati.

Related Articles

Back to top button