Mastaa

Wakili wa Sean ‘Diddy’ Combs’ ajibu kukamatwa mafuta ya watoto

NEW YORK: WAKILI wa hitmaker wa ‘I’ll Be Missing You’, Marc Agnifilo Ameshangazwa na wingi wa chupa za mafuta ya Watoto zilizotajwa kupatikana nyumbani kwa mteja wake ambaye ni mwanamuziki na mfanyabiashara, Sean ‘Diddy’ Combs.

Wakili huyo amesema hakukuwa na ulazima wa kuwa na chupa nyingi hivyo wakati chupa moja inaweza kutumika kwa muda mrefu hivyo katika nyumba ya mteja wake hakukuwa na chupa 1,000.

Kwa mujibu wa mamlaka Sean ‘Diddy’ Combs alikuwa na zaidi ya chupa 1,000 za mafuta ya watoto nyumbani kwake.

Mkali huyo wa muziki wa rap mwenye umri wa miaka 54 alikamatwa wiki iliyopita na kushtakiwa kwa biashara ya ngono, ulaghai na usafirishaji ili kufanya ukahaba, huku ripoti zikieleza vitu mbalimbali ambavyo polisi walivikamata wakati nyumba yake ilipovamiwa mapema mwaka hii.

Wakili huyo aliiambia TMZ katika mazungumzo ya filamu yao ya awali ‘The Downfall of Diddy: The Indictment’: “Sijui Chupa 1,000 ziilikujaje?

“Nina hakika mafuta ya watoto hayana uhusiano na chochote kwenye mashitaka yake.”

Alipoambiwa nambari hiyo ilitoka moja kwa moja kutoka kwa hati za serikali na kupendekeza mafuta yalikuwa yametumiwa wakati wa matukio kadhaa, wakili huyo aliongeza: “Nadhani. Sijui unahitaji chupa1,000 za nini wakati chupa moja ya mafuta ya mtoto hutumika kwa muda mrefu. Sijui ungehitaji chupa 1,000 kwa ajili gani?

“Sidhani kama ilikuwa elfu. Nadhani yalikuwa mengi hebu yalikuwa mengi,” huku wakili wa rapper akipuuza madai hayo.

Mahali pengine katika makaratasi, ilijadili kukamatwa kwa mafuta ya watoto.

Karibu Machi 2024, wakati wa upekuzi wa makazi ya Combs huko Miami, Florida na Los Angeles, California, Wenye Malaka walinasa vifaa mbalimbali zikiwemo chupa 1,000 za mafuta ya watoto. Diddy amekana mashitaka yote yanayomkabili.

Related Articles

Back to top button