Mastaa

Angelina Jolie: Nipo tayari kuchumbiwa tena

NEW YORK: BAADA ya kuhisiwa kutoka kimapenzi na rapa Akala, mcheza filamu mashuhuri nchini Marekani, Angelina Jolie ameweka wazi kwamba kwa sasa yupo tayari kuchumbiwa tena baada ya kuachana na aliyekuwa mume wake Brad Pitt.

Taarifa zilizozagaa katika mitandao mingi nchini humo zinadai kwamba Angelina na rapa Akala. Kwa wiki kadhaa, wameonekana wakiwa pamoja na ripoti pia zimedai kwamba walitumia muda pamoja kwenye hoteli yake huko London hivi karibuni.

Ripoti mpya ya In ‘Touch Weekly’ inanukuu chanzo cha karibu na mwigizaji huyo, akisema, “Angie yuko tayari kuchumbiana tena, ingawa haijulikani ikiwa yeye na Akala kuna uhusiano wa kweli ama la lakini yeyote atakayechumbiana naye baadaye atalazimika kufuata masharti yake.

Alipoulizwa ni masharti gani mtu huyo wa karibu alijibu “Angelina kwake, watoto huja kwanza. Yeye pia anataka kubembelezwa. Angie amepitia mengi tangu alipowasilisha maombi ya talaka kutoka kwa Brad Pitt. Kwa sasa hataki kitu kingine zaidi ya kuchumbiwa tena lakini atakayemchumbia lazima afuate masharti yake hayo ya watoto wake kwanza na ajue kumbembeleza,”

Angelina Jolie ana watoto sita wenye umri wa miaka 16 hadi 23 watatu kati yao Angelina alikuwa akiwalea kabla ya kuolewa na Brad Pitt.

Angelina na Brad walianza kuchumbiana baada ya kukutana kwenye seti za Mr & Mrs. Smith mwaka wa 2005. Wenzi hao walioana mwaka 2014 lakini walitengana miaka miwili baadaye. Talaka yao ilikamilishwa mnamo 2019. Lakini wawili hao wameingia kwenye vita vya kisheria kuhusu madai ya unyanyasaji wa maneno na kimwili na mzozo wa mali.

Hivi majuzi Angelina alirudi kwa ushindi kwenye filamu kwa mwaka huu ya Maria Callas. Filamu hiyo imeongozwa na Pablo Larraín, ilionyeshwa kwa mara ya kwanza kwenye Tamasha la 81 la Kimataifa la Filamu la Venice mnamo Agosti na kupokea maoni chanya.

Angelina katika filamu ya Maria umesifiwa na mwigizaji huyo anachukuliwa kuwa mtangulizi wa tuzo za Oscar mwaka huu. Filamu hiyo itakuwa na toleo fupi katika kumbi za sinema mnamo Novemba kabla ya kutolewa kwenye Netflix mnamo Desemba 11.

Related Articles

Back to top button