Africa

Yei Joint Stars ya Sudan Kusini yafuzu nusu fainali CECAFA

TIMU ya wanawake ya Yei Joint Stars kutoka Sudan Kusini imefuzu hatua ya nusu fainali ya mashindano ya CAF Women’s Champions League CECAFA Qualifiers 2026, yanayofanyika jijini Kigali, Rwanda

Yei Joint Stars imekuwa timu ya kwanza kufuzu hatua hiyo baada ya kupata ushindi wa mabao 1-0 dhidi ya Mafunzo Queens ya Zanzibar katika mchezo wa Kundi A uliochezwa Uwanja wa Kigali Pelé, Kigali nchini Rwanda.

Goli pekee la mchezo huo lilifungwa na Mary Anger Bol dakika ya 69, baada ya Yei Joint Stars kufanya shambulizi lililozaa nafasi iliyowezesha mshambuliaji huyo kuipatia timu yake ushindi.

Ushindi huo ulikuwa wa pili mfululizo kwa Yei Joint Stars baada ya kuanza mashindano kwa kuifunga Denden FC ya Eritrea mabao 3-0, hivyo kufikisha pointi sita na kujihakikishia nafasi ya kucheza nusu fainali.

Mashindano hayo yanafanyika kuanzia Agosti 21 hadi 31, 2026, jijini Kigali, Rwanda, yakishirikisha timu 10 kutoka ukanda wa CECAFA. Michezo inachezwa katika Kigali Pelé Stadium na FERWAFA Technical Centre.

Related Articles

Back to top button