Africa

Mzamiru: Sfaxien sio wepesi ila tutawapiga

TUNISIA: KIUNGO wa Simba Mzamiru Yassin amesema mechi yao ya Kombe la Shirikisho Afrika (CAF CC) dhidi ya Sfaxien ya Tunisia haitakuwa nyepesi wanahitaji jitihada, umakini na nguvu kuhakikisha wanapata matokeo.

Simba watacheza na Sfaxien kesho kutwa Jumapili nchini Tunisia mchezo wa nne hatua ya makundi.

Akizungumza katika mazoezi yao nchini Tunisia Mzamiru amesema licha ya wapinzani wao kushika mkia kwenye kundi haimaanishi ni wepesi bado mchezo unaweza kuwa mgumu hivyo, hawapaswi kubweteka.

“Mechi za ugenini huwa ni ngumu haijalishi umecheza na timu gani tunatakiwa tuwe makini, mtu anapopata dakika za kucheza ajitoe kwa kuonesha jitihada za hali ya juu kuisaidia timu.

“Wapinzani wetu hawajapata matokeo sio kwamba ni wabaya bado tunapaswa kuwaheshimu, ni mechi ngumu inayohitaji umakini, kwa jitihada zetu na nguvu zetu tunaweza kupata ushindi,”amesema.

Amesema hawapaswi kusubiri mechi ya mwisho ndio iamue matokeo lazima wachukulie kila mchezo kama fainali na kupata matokeo mazuri ili michezo inayokuja mbele iweze kuwa rahisi zaidi.

Wekundu hao wa Msimbazi wako kundi A wakishika nafasi ya tatu baada ya kucheza michezo mitatu na kati ya hiyo, kushinda miwili, kupoteza mmoja wakiwa na pointi sita sawa na kinara Bravos ya Angola na CS Constatine ya Algeria nafasi ya pili kukiwa na utofauti wa mabao ya kufunga na kufungwa.

Related Articles

Back to top button