Muziki

‘Only Jesus Know’ yampaisha Relie Afrika Mashariki

CAMEROON: MSANII wa muziki wa Injili kutoka Cameroon, Relie M, amewashukuru mashabiki wa Afrika Mashariki kwa mapokezi makubwa ya wimbo wake mpya wa rap, Only Jesus Know.

Akizungumza na SportLeo, Relie M amesema ndani ya muda mfupi tangu kuachiwa kwa wimbo huo, Only Jesus Know imefanikiwa kupata wasikilizaji na watazamaji wengi kutoka ukanda huu.

“Only Jesus Know imenifungulia njia zaidi huko Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla.

Nimepata idadi kubwa ya watazamaji kwenye chaneli yangu ya YouTube, naamini mashabiki wanaendelea kunipa sapoti ili kwa pamoja muziki wetu ufike mbali,” amesema Relie M.

Binti huyo mdogo anayekuja kwa kasi kwenye muziki wa Injili barani Afrika anasimamiwa na Rim Plug ya Rene Immortal chini ya lebo ya Queen Light Music.

Related Articles

Back to top button