Ligi Kuu

Iddy Nado: Ibenge alitaka alama tatu kwa namna yoyote

DAE ES SALAAM: NYOTA wa Azam, Seleman Iddy ‘Nado’ amesema kocha wa timu hiyo,  Florent Ibenge aliwataka kuhakikisha wanapata alama tatukipindi cha pili kwa namna yoyote.

Kauli hiyo ya kocha iliwapa motisha wachezaji na hatimaye wakafanikiwa kupata goli la pili lililowapatia ushindi kupitia mkwaju wa penati.

Nado amesema baada ya kushindwa kupata alama hizo katika kipindi cha kwanza, kocha Ibenge aliwataka kurejea kipindi cha pili wakiwa na dhamira ya kupata ushindi.

Nado alikuwa miongoni mwa wachezaji waliohusika moja kwa moja katika ushindi huo, akitoa pasi iliyozalisha goli la kwanza la timu yake.

Mbali na kutoa pasi hiyo, Nado pia alisababisha penati iliyozalisha goli la pili, hivyo kuwa mhimili muhimu katika ushindi wa timu yake na kuibuka mchezaji bora wa mchezo.

“Kocha alituambia kama tumeshindwa kupata pointi tatu kipindi cha kwanza, tukirudi dakika 45 za kipindi cha pili tuhakikishe tunapata alama tatu kwa njia yoyote ile. Nasi tumefanikiwa kupata alama tatu, tunafuraha na tunamshukuru Mungu,” amesema Nado.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button