Africa

Simba yarejesha heshima ya nchi

DAR ES SALAAM: BAO la mkwaju wa penati la kiungo mshambuliaji wa Simba Charles Ahoua dakika ya 27 limeipa Simba ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Bravos do Maquis katika mchezo wa kombe la Shirikisho Afrika leo Uwanja wa Benjamin Mkapa Dar es Salaam.

Kipa wa Simba, Moussa Camara amekuwa shujaa kwa kudaka penati dakika ya 47 iliyopigwa na mchezaji wa Bravos do Maquis, Emmanuel Edmond.

Simba wameanza na mguu mzuri kwenye michuano hiyo na kufuta machungu ya Taifa mara baada ya jana wawakilishi wa Tanzania kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika Yanga kufungwa mabao 2-0 na Al Hilal ya Sudan.

Ushindi wa Simba umeendele kuonesha ukomavu wa miamba hiyo ya Kariakoo linapokuja suala la michezo ya Kimataifa kwani wamekuwa watofauti kwenye ushiriki wao katika michuano hiyo.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button