AFCONAfrica

Tanzania, Uganda na Kenya wenyeji AFCON 2027

Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) limepitisha ombi la pamoja la Tanzania, Uganda na Kenya kuandaa fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2027.

Rais wa CAF Patrice Motsepe ametangaza Ombi la Pamoja la Afrika Mashariki kuwa washindi wa haki ya kuandaa michuano hiyo baada ya mkutano wa Kamati Tendaji ya shirikisho hilo uliofanyika leo mji mkuu wa Misri, Cairo.

Fainali za AFCON 2023 zitafanyika Ivory Coast wakati za mwaka 2025 zitafanyika Morocco.

Tayari Tanzania, Uganda na Kenya zimeanza maandalizi kwa ajili ya AFCON 2027.

 

 

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button