Ligi KuuNyumbani

Yanga yaipania Geita

KOCHA Msaidizi wa Yanga, Cedric Kaze amesema kitu kikubwa na malengo ya klabu hiyo ni alama tatu kwenye kila mchezo.

Akizungumza leo jijini Mwanza kuelekea mchezo wa Ligi Kuu ya soka Tanzania Bara dhidi ya Geita Gold Oktoba 29 Kaze amesema mchezo huo ni mgumu lakini lengo la pointi 3 lipo palepale.

“Tunaingia kwenye kila mchezo kwa malengo hatuingii kwenye mechi kwa sababu ya kuendeleza takwimu ya kucheza bila kupoteza maana unaweza usipoteze mechi lakini ukakosa kutimiza malengo ya klabu,” amesema Kaze.

Kocha huyo amesema klabu inalazimika kufanya mabadiliko ya wachezaji kutokana na michezo mingi katika kipindi kufupi.

“Tukicheza mchezo wa kesho tunakuwa tumecheza mechi nne ndani siku kumi, hakuna mwili wa binadamu unaweza kuhimili hili na ndio maana mnaona baadhi ya michezo tunafanya mabadiliko lakini tunahakikisha hayaathiri utendaji na malengo kwenye kipindi hiki kigumu,” amesema.

Related Articles

Back to top button