Ligi Kuu

Abdulrazack tayari kuivaa Yanga

DAR ES SALAAM:BEKI wa Simba, Abdulrazack Hamza amerejea kikosini kuanza mazoezi baada ya kupata jeraha katika mchezo uliopita dhidi ya Coastal Union.

Akizungumza na Spotileo, Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Simba, Ahmed Ally amesema Abdulrazack ameimarika na ameingia kambini kuendelea na maandalizi ya Kariakoo Derby, inayotarajiwa kucheza Jumamosi Oktoba 19.

“Abdulrazack alipata jeraha dogo katika mchezo uliopita dhidi ya Coastal Union, alipewa matibabu na sasa yupo fiti na anaendelea mazoezi kuelekea mechi ijayo,” amesema Ahmed.

Ameeleza kuwa wachezaji waliopo katika majukumu ya timu za taifa akiwemo kipa, Moussa Camara anarejea mapema Dar es Salaam baada ya Kumaliza majukumu yake ya timu ya taifa akiwa na Guinea.

Camara alicheza dakika zote 90 katika mechi zote mbili dhidi ya Ethiopia, ambapo Guinea ilishinda 4-0 na 3-0, anarejea Tanzania kuendelea na majukumu yake akiwa na Simba.

Steven Mukwala pia anatarajiwa kuwasili Tanzania mchana wa leo, Kibu Denis, Mohammed Hussein watakuwa sehemu ya mazoezi ya leo jioni.

Related Articles

Back to top button