Ligi Kuu
Pamba Jiji VS Simba; nje vita ndani vita

MWANZA: Baada ya mapumziko ya kupisha michezo ya kimataifa. Ligi kuu ya NBC inatarajia kuendelea leo kwa mchezo mmoja ambapo wenyeji wa dimba la CCM kirumba jijini Mwanza, Pamba jiji watakuwa dimbani hapo kuwakabili Mfalme wa nyika na vinara wa ligi hiyo Simba SC kutoka jijini Dar Es Salaam.
Mchezo huo unaotarajiwa kupigwa saa 10 jioni unatarajia kuwa na mvuto wa aina yake kutokana na mazingira ya nje ya uwanja kuelekea mchezo huo.
Simba SC walilalamika kufanyiwa vurugu mazoezini na wenyeji wao hao wakiongozwa na mkuu wa mkoa huo Said Mtanda jambo ambalo ofisi ya mkuu wa mkoa Mwanza imekanusha vikali wakisema ‘bosi’ huyo alienda CCM kirumba hapo kwa ajili ya kuwatoa uwanjani maafisa wa Pamba ambao walikuwa wamefungiwa uwanjani hapo.