Nyumbani

yanga Wamelipa kujaza kwa Mkapa

DAR ES SALAAM: Wamelipa!. Mashabiki wa Yanga wamefanikiwa kujaza uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam unaochukuwa mashabiki 60,000, kusherehekea kilele cha wiki ya Wananchi.
 
Mashabiki hao walifurika katika uwanja huo asubuhi kuanzia saa 3:00 asubuhi kwenye eneo la uwanja huo uliopo manispaa ya Temeke jijini humo kushuhudia timu yao ikicheza mechi ya kirafiki dhidi ya Red Arrows ya Zambia.
 
Kabla ya kuanza kwa burudani, kulikuwa na mechi ya kirafiki kati ya timu ya mchanganyiko wa viongozi na wachezaji wa zamani wa Yanga dhidi ya mashabiki wa timu hiyo.
 
Baada ya hapo mashabiki walipata burudani ya muziki kutoka kwa wasanii mbalimbali ikiwemo msanii wa muziki wa kizazi kipya Harmonize kuimba nyimbo maalum ya kuwasifia wachezaji wa klabu hiyo ya mtaa wa Twiga na Jangwani.
 
Muda mchache ujao Yanga wanatarajia kukitambulisha rasmi kikosi chao cha msimu mpya wa 2024/25 pamoja na kucheza mechi ya kirafiki dhidi ya Red Arrows ya Zambia majira ya saa 1: 00 usiku
 

Related Articles

Back to top button