
LIGI Kuu ya Soka Tanzania inaendelea leo kwa mchezo mmoja kufanyika uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.
Mchezo huo unazikutanisha timu za watoza ushuru, klabu ya Manispaa ya Kinondoni, KMC dhidi ya Mbeya City ya jiji la Mbeya.
Mbeya City inashika nafasi ya 7 katika msimamo wa ligi ikiwa na pointi 19 baada ya michezo 14 wakati KMC ipo nafasi ya 10 ikiwa na pointi 15 baada ya michezo 14.
Novemba 30 kumefanyika mchezo mmoja wa ligi hiyo kwenye uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga ambapo wenyeji Coastal Union imejikuta ikipata kipigo cha bao 1-0 kutoka kwa Dodoma jiji.