Ligi KuuNyumbani

Tanzania Prisons kusajili wanne

KOCHA Mkuu wa Tanzania Prisons, Patrick Odhiambo timu hiyo imepanga kusajili wachezaji wasiopungua wanne kwenye dirisha dogo la usajili ili kuimarisha kikosi cha maafande hao.

Akizungumza na SpotiLeo, kocha huyo raia wa Kenya amesema katika wachezaji hao wanne wawili wakiwa wa kigeni.

“Nimeshauambia uongozi wangu na umekubali kwa sasa wawakilishi wetu wemeshaanza mazungumzo na nyota hao ambao tumekusudia kuwaongeza kwenye kikosi chetu,” amesema Odhiambo.

Kocha huyo amesema nafasi ambazo amepanga kuziboresha ni ushambuliaji, kiungo wa juu na beki mmoja wa kati.

Tanzania Prisons ipo nafasi ya 11 kwenye msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara ikikusanya pointi 21 baada ya michezo 18.

Related Articles

Back to top button