Burudani

Willy Paul awaomba radhi Bahati na mkewe

NAIROBI: MSANII wa Kenya Willy Paul amemuomba msamaha mwanamuziki Bahati na mkewe, Diana Marua kwa alichowakosea.

Katika ujumbe alioandoka katika mtandao wake wa kijamii, Willy Paul amekiri kuwakosea Bahati mara kadhaa na amejutia alichokifanya.

“Vitendo vyangu havikukusudiwa kufanyika, lakini sijui walichukuliaje. Ninaomba msamaha wa dhati kwa Diana na watoto wao kwa kutokuelewana.

Katika majibu wa Bahati amekubali msamaha hadharani, akisema, “Msamaha ulikubaliwa,” na wakathibitisha dhamana yao ya kindugu.

“Ndugu yangu @willy.paul.msafi, Msamaha ulikubaliwa. Tumetoka mbali, tukishinda umaskini katika makazi duni ya Mathare kuwa sisi ni nani leo. Makosa hufanyika, lakini mambo muhimu ni kurekebisha. Hakuna makosa makubwa,” ameandika Bahati.

Mashabiki wamesifu maridhiano yao huku wakiwataka kuimba wimbo wa kushirikiana. Diana Marua alikuwa amechukua hatua za kisheria dhidi ya Willy Paul, lakini baada ya msamaha huo kesi hiyo imefutwa.

Related Articles

Back to top button