Burudani

Harmonize: Marufuku kupiga wimbo wa Yanga bingwa

DAR ES SALAM: MSANII wa Bongo Fleva, Harmonize amezuia wimbo wake wa ‘Yanga Bingwa’ kupigwa sehemu yoyote hadi pale atakapotoa taarifa.

Sambamba na hilo, Harmonize ameoneshwa kuchukizwa na msanii Tundaman kutumia wimbo wake huo bila kumpa taarifa yoyote.

““Warning sitaki wimbo wangu wa ‘Yanga Bingwa’ upigwe sehemu yoyote sio kumbi za starehe wala sehemu yoyote yenye mkusanyiko mpaka nitakapo wajulisha asanteni sana natarajia ushirikiano ndugu DJS ngoma za kupiga ni nyingi mno pigeni hii mpya ya Nandy” ameandika Harmonize katika ‘Insta story yake’.

Wimbo wa Yanga bingwa uliachiwa na msanii huyo miezi mitatu iliyopita ukiwa ni wimbo maalumu wa kuwakaribisha wachezaji wapya na kuanza msimu mpya wa 2024/25.

Related Articles

Back to top button