Wema: Niliambulia manukato tu kutoka kwa Idris Sultan

DAR ES SALAAM:
ALIYEKUWA Miss Tanzania Wema Sepetu amekana kutumia fedha za aliyekuwa mpenzi wake Indris Sultan baada ya kushinda shindano la Big Brother Africa miaka michache iliyopita.
Idris Sultan ambaye ni mshiriki wa zamani wa Big Brother Africa alikuwa na mahusiano ya kimapenzi na Wema Sepetu mwishoni mwa 2015 na 2016.
Sultan alishinda fedha nyingi ambazo tuhuma nyingi zilielekezwa kwa Wema Sepetu kwamba ndiye alitumia fedha za msanii huyo wa filamu na sanaa ya uchekeshaji.
“Inaniuma sana wakati watu wanatembea na kunishutumu kwa kufuja pesa zake. Sikuwahi kuchukua hata shilingi moja kutoka kwake. Kama nilipata chochote kutoka kwake, ilikuwa ni zawadi ya manukato ya Tom Ford, si kitu kingine chochote, naye anaweza kushuhudia jambo hilo. Anajua jinsi alivyopoteza pesa zake, sikuwa sehemu yake. Aliyefurahia pesa ni Samantha walipokuwa pamoja, sio mimi.” Ameeleza Wema Sepetu.
Wema anasema anatamani Idris angeshughulikia suala hilo ili kuepuka watu kuendelea kuchafua jian lake.
“Hata yeye anashangaa kwa nini huwa nalalamikiwa kutumia fedha zake. Hawezi kujitokeza hadharani kunitetea kwa sababu hatuko pamoja tena, lakini nadhani lingekuwa jambo la busara kwake kujitokeza na kuzima shutuma hizi zote za jambo hilo,”
Baada ya kuachana na Idriss, Wema aliendelea kutamba katika uhusiano na watu mbalimbali akiwemo Diamond Platnumz kisha kuachana. Wema kwa sasa yupo katika mahusiano na Whozu.