Riadha

Vipaji vya riadha vyang’aa Dar

DAR ES SALAAM:MWENYEKITI wa Chama cha Riadha Mkoa wa Dar es Salaam, Amani Ngoka, amesema mashindano ya vijana yanayoendelea jijini humo yameanza kuonesha mwanga mkubwa wa kupata vipaji vya baadaye kwa ajili ya timu za taifa.

Akizungumza na SpotiLeo, Ngoka amesema mwitikio wa vijana umeanza vizuri na anaamini hadi kesho vipaji vingi vitaendelea kuibuka.

Amesema kwa ujumla ushiriki wa wavulana na wasichana umeonekana kuwa wa kuridhisha, ingawa bado idadi ya wasichana si kubwa sana kama inavyotarajiwa.

“Uwiano umeenda vizuri, ila wasichana sio wengi sana. Tunawaomba wazazi wawaachie watoto waje kuonesha vipaji vyao, nasi tutawalea katika maadili na michezo,” ameongeza.

Ngoka amesema mashindano hayo yanaweza kuwa chachu kwa mikoa mingine kuanzisha mfumo kama huo ili kusaidia kupata vijana wengi watakaokuja kuitumikia timu ya taifa hapo baadaye.

Kwa upande wake, mmoja wa washiriki wa mashindano hayo, Ramadhan Hamis kutoka Kimara, amesema ameridhishwa na kiwango cha ushindani baada ya kushika nafasi ya kwanza katika mbio za mita 800.

Ramadhan amesema amekuwa akivutiwa na mwanariadha wa Tanzania Alphonce Simbu, ambaye amekuwa chanzo cha hamasa kwake kushiriki riadha.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button