Riadha

Mkenya avuna medali ya dhahabu na dola 50,000 Olimpiki 2024

PARIS:MWANARIADHA wa Kenya Beatrice Chebet kutoka Kenya ameipa nchi yake medali ya kwanza ya dhahabu baada ya kuonesha kiwango bora kilichochangia kushinda fainali ya mbio za mita 5,000 kwa wanawake katika michezo ya Olimpiki ya Paris ya mwaka 2024 nchini Ufaransa.

 

Chebet alitumia muda wa dakika 14:28.56 baada ya kumshinda mkenya mwenzake Faith Kipyegon, ambaye alishika nafasi ya pili na kunyakua medali ya fedha.

 

Chebet atakimbia katika fainali ya mita 10,000 zitakazofanyika Ijumaa, Agosti 9, na kwa kuwa riadha ya Dunia ilianzisha tuzo na zawadi za fedha kwa watakaoshinda medali za dhahabu kwa hiyo Chebet atapata dola 50,000 ambazo ni sawa na Shmilioni 135 za Tanzania.

 

Chebet alimaliza nyuma ya Kipyegon na Hassan katika Mashindano ya Dunia ya riadha ya mwaka 2023 yaliyofanyika huko Budapest.

 

Endapo atashinda tena mbio za mita 10,000 zinazotarajiwa kufanyika Siku ya Ijumaa atakuwa ameiwezesha Kenya kushinda medali mbili za dhahabu na yeye atajizolea kitita cha pesa zaidi kutoka kwa kamati ya mashindano hayo.

 

Kipyegon, Gudaf Tsegay na bingwa mtetezi Sifan Hassan walikuwa wakipigiwa upatu kushinda nafasi hiyo lakini Chebet ndiye aliibuka mshindi katika mbio hizo kwa kukimbia kwa kasi na rekodi ya dunia.

Related Articles

Back to top button