Mnyanyua vitu vizito kutoka India aandika historia mpya Jumuiya ya Madola

GLASGOW: Mnyanyua vitu vizito wa India, Mirabai Chanu, ameendelea kuandika historia baada ya kutwaa medali ya dhahabu katika mashindano ya Jumuiya ya madola 2026, ushindi uliompa taji lake la tatu mfululizo kwenye michezo hiyo.
Chanu alitawala mashindano ya uzani wa kilo 48 kwa kuonesha ubora mkubwa dhidi ya wapinzani wake, akiipa India medali yake ya kwanza ya dhahabu katika toleo la mwaka huu la michezo hiyo.

Baada ya ushindi huo, Chanu alishindwa kujizuia na kububujikwa machozi wakati wimbo wa taifa la India ulipopigwa, akieleza kuwa mafanikio hayo yana thamani kubwa kwake baada ya kupitia kipindi kigumu cha maandalizi.
Ushindi wake umeongeza matumaini kwa India kuendelea kukusanya medali zaidi, huku Australia ikiendelea kuongoza jedwali la medali katika siku za mwanzo za mashindano yanayoendelea jijini Glasgow.
Jumuiya ya madola 2026 zinawakutanisha zaidi ya wanamichezo 3,000 kutoka mataifa 74 ya Jumuiya ya Madola wakishindana katika michezo mbalimbali hadi Agosti 2.



