Riadha

Mkenya Mary Moraa ashinda tuzo Zurich

ZURICH: MWANARIADHA kutoka Kenya, Mary Moraa ameshinda mbio za mita 800 za wanawake katika mbio za Zurich Diamond League zilizofanyika Jana Septemba 5.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24 alitumia saa 1:57.08 na kushinda mbio hizo mbele ya Georgia Bell aliyetumia 1:57.94 na kushinda nafasi ya pili huku Wiley Addison aliyetumia 1:58.16 akishika nafasi ya tatu.

Mary aliwahi kuvunja rekodi ya dunia katika mbio za mita 600 za wanawake katika mbio za ISTAF zilizofanyika mjini Berlin, Ujerumani.

Alitumia sekunde 0.14 kutoka kwa rekodi ya Caster Semenya ambayo ilikuwa imesimama bila kuvunjwa tangu 2017.

Shafiqua Maloney alitawala mkondo wa kwanza wa mbio hizo lakini hakufanikiwa kumshinda mkenya huyo.

Moraa katika mbio za Michezo ya Olimpiki iliyofanyika Paris, Ufaransa kwa jina la Nyamira Express au Malkia wa Dansi, Moraa alikuwa wa tatu akimaliza nyuma ya Keely Hodgkinson wa Uingereza na Tsige Duguma wa Ethiopia.

Kuelekea Weltklasse, Moraa tayari amejihakikishia nafasi yake katika fainali mjini Brussels wiki ijayo. Hii itakuwa mechi yake ya nne ya Diamond League katika mbio za mita 800.

Related Articles

Back to top button