Habari Mpya

Uchafuzi wa maji waahirisha mbio za maji Olimpiki 2024

PARIS: UCHAFUZI wa mazingira katika mto Seine umelazimisha waandaaji wa Olimpiki 2024 kuahirisha shindano la mbio za maji kwa wanaume hadi kesho Julai 31.

Kushindikana kufanyika kwa shindano hilo kumetishia kuharibu juhudi kubwa za waandaaji wa michezo hiyo ya Olimpiki waliotenga dola za Marekani 1.5 bilioni kwa ajili ya kusafisha njia yam aji hayo machafu iliyopita katikati ya jiji la Paris.

Taarifa iliyotolewa na Paris 2024 ilisema vipimo vilionyesha ubora wa maji katika mto huo wa Seine bado uko chini ya kiwango kinachokubalika kwa wanariadha na waogeleaji kufanyia mashindano yao.

Mbio za wanaume zimeahirishwa hadi Jumatano saa 10:45 kwa saa za huko (4:45 a.m. ET), mara baada ya tukio la wanawake, ambalo limepangwa kufanyika saa mbili asubuhi.

“Kwa bahati mbaya, matukio ya hali ya hewa nje ya uwezo wetu, kama vile mvua iliyonyesha Paris mnamo tarehe 26 na 27 Julai, inaweza kubadilisha ubora wa maji na kutulazimisha kupanga upya tukio hilo kwa sababu za kiafya,” taarifa ilieleza.

“Licha ya uboreshaji wa viwango vya ubora wa maji katika saa za mwisho, usomaji katika baadhi ya maeneo ya kozi ya kuogelea bado uko juu ya mipaka inayokubalika.”

Related Articles

Back to top button