Kwingineko

Tuchel kutoimba wimbo wa taifa wa England

LONDON, Meneja wa kikosi cha The three Lions timu ya taifa ya England raia wa Ujerumani Thomas Tuchel amesema ni lazima ‘apate haki’ ya kuimba wimbo wa taifa hilo katika mechi za kufuzu kombe la dunia la 2026 kati ya kikosi chake na Latvia na Albania

Tuchel mwenye miaka 51 aliyesema hayo wakati akijibu swali la mwandishi wa habari katika mkutano wake wa kutangaza kikosi kitakachocheza michezo hiyo akitaka kujua kama ataimba wimbo huo maarufu wa ‘God save the King’ na akajibu hataimba.

“Nadhani natakiwa kupata haki kwanza, huwezi kuimba tu wimbo wa taifa, ndio maana nimeamua sitaimba wimbo huo katika michezo yangu ya kwanza na timu hii”

“Kwanza, Nadhani unapaswa kuwa na nguvu na hisia za uzalendo ili uuimbe wimbo wa taifa vizuri na mimi sijafanya chochote cha kujivunia kwa taifa hili kiasi cha kuimba wimbo wa taifa, anajihisi bado hivyo sitaimba. Nawahakikishia hakuna kitu kinachotakiwa kufanywa kwa nguvu zote na uzalendo kama wimbo wa taifa na mimi nitaitafuta haki ya kuimba uwanjani” amesema Tuchel

Baada ya kuteuliwa, meneja huyo wa zamani wa Chelsea na Bayern Munich ataiongoza timu hiyo kwa mara ya kwanza kwenye mchezo dhidi ya Albania machi 21. Awali wakati wa uteuzi wake mwezi Oktoba mwaka jana alisema hajaamua iwapo ataimba wimbo huo au la.

Tuchel alichukua rasmi mikoba ya kuinoa timu ya taifa ya England Januari mosi mwaka huu

Related Articles

Back to top button