Kwingineko

Ancelotti: nimemchoka Guardiola

MADRID:MENEJA wa mabingwa watetezi wa Ligi ya Mabingwa barani Ulaya Real Madrid, Carlo Ancelotti amesema amechoka kucheza dhidi ya meneja mwenzake wa Manchester City Pep Guardiola mara kwa mara.

Ancelotti ameyasema hayo baada ya mwandishi wa TNT Sports kumuuliza hisia zake juu ya kukutana na Pep Guardiola kwa mara ya 10 kwenye Ligi ya Mabingwa, wakiwa ni mameneja pekee wa timu kukutana mara nyingi zaidi kwenye michuano hiyo.

“Nimechoka, kwakweli nimechoka lakini bado nadhani Guardiola ni miongoni mwa mameneja bora sana kuwahi kukutana nao lakini nimechoka kucheza dhidi yake, nimechoka sana lakini huwa najisikia poa kukutana nae wakati wote” – Amesema Ancelotti

Alipoulizwa kuhusu utofauti na changamoto mpya kila wanapokutana Ancelotti amesema hakuwezi kuwa na tofauti kwa sababu hawakutani Carlo Ancelotti na Pep Guardiola bali ni Real Madrid na Manchester City.

“Hapana sidhani kama suala ni kuna changamoto mpya au la kwa sababu huwa hatuchezi mimi na yeye ni Real Madrid na Manchester City zenye vikosi vilivyojaa wachezaji wenye vipaji vya hali ya juu” – ameongeza

Real Madrid walio na uongozi wa 3-2 kwenye ‘aggregate’ watawakaribisha Santiago Bernabeu wababe wenzao Manchester City kwenye mchezo wa mzunguko wa pili wa kuwania hatua ya 16 bora ya UEFA Champions League leo saa 5 usiku saa za Afrika Mashariki.

Related Articles

Back to top button