TRA kuhamishia hasira kwa Dodoma Jiji

ARUSHA:KOCHA Mkuu wa TRA, Etienne Ndayiragije, amesema kikosi chake kimejiandaa vyema kukabiliana na Dodoma Jiji katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara utakaochezwa kesho, kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid mkoani Arusha.
Ndayiragije amesema wamewasili jioni mkoani hapa na kufanya maandalizi mepesi yaliyolenga kuwapa wachezaji nafasi ya kurejea katika hali nzuri baada ya safari, huku akieleza kuwa baadhi ya wachezaji wanaendelea kusumbuliwa na majeraha.
“Tumefika jioni, tukaweza kufanya mazoezi kidogo, kurejesha mwili katika hali yake na kufanya maandalizi yetu. Kuna majeruhi, lakini wote tupo kwenye imani kwamba tutafanya vizuri katika mchezo wa kesho wa nyumbani. Mungu atubariki tuweze kupata matokeo mazuri,” amesema.
Kocha huyo amesema matokeo ya mchezo huo yataakisi kiwango cha utendaji wa timu yake, akisisitiza kuwa wachezaji wanapaswa kuonesha kile walichojiandaa nacho uwanjani.
“Ni sare tumepata au tumepoteza, kinachobaki ni wachezaji kuonesha matarajio yao. Matokeo yanafuatana na utendaji. Sisi kama wachezaji tumejiandaa vizuri kwa mchezo wa kesho. Najua ni mchezo mgumu, lakini tumejiandaa kwa ajili ya mchezo huo,” amesema Daniel Mgore.
“Tunajua ni mchezo mgumu, lakini tumejiandaa vizuri kwa ajili ya mchezo wa kesho. Tunatarajia kufanya vizuri na kupata matokeo mazuri mbele ya mashabiki wetu,” amesema Mgore.




