Ligi Kuu

Barker: Tulistahili kushinda

DAR ES SALAAM:KOCHA wa Simba, Steven Barker, amesema timu yake ilistahili kuibuka na ushindi katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Coastal Union, licha ya kupata ushindi wa bao 1-0.

Barker amesema Simba ilitawala mchezo kwa kiasi kikubwa na kuifanya Coastal Union kushindwa kupata nafasi nyingi za kutengeneza mashambulizi, akieleza kuwa wapinzani wao hawakuwa na kona wala shuti lililolenga lango.

“Namna tulivyoutawala mchezo ilikuwa ya kipekee. Sidhani kama walipata hata kona moja, wala sikumbuki ‘free kick’au shuti lililolenga lango. Kwa hiyo wakati mwingine unatawala mchezo na kucheza vizuri kama tulivyofanya leo, lakini hupati matokeo makubwa zaidi,” amesema Barker.

Kwa upande wake, Kocha wa Coastal Union, Fikiri Elias, amesema Simba ilikuwa mtihani mzuri kwa vijana wake, huku akieleza kuwa mpango wao ulikuwa kucheza kwa nidhamu kabla ya kutumia nafasi za kushambulia kwa haraka kupitia njia.

Elias amesema vijana wake walitekeleza vizuri mpango huo hadi dakika za mwisho, kabla ya makosa ya mawasiliano kati ya kipa na mabeki kuipa Simba nafasi ya kupata bao lililoamua mchezo. Amesema sasa kazi kubwa ni kuboresha namna ya kutoka haraka kwenda kushambulia baada ya kujilinda.

“Tumetaka vijana wetu wawe karibu, lakini pia wawakamate Simba kwenye njia. Tumejaribu kufanya hivyo mara kwa mara, ingawa haikuwa rahisi. Vijana wamejitahidi sana kudumisha nidhamu hiyo hadi karibu dakika ya 80, lakini kutokana na makosa ya mtu mmoja mmoja na mawasiliano kati ya kipa na beki, Simba ikapata nafasi na kufunga,” amesema Elias.

 

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button