Ligi Kuu

Koplo Bacca amchana Ateba!

BEKI wa Yanga, Ibrahim Bacca amemtumia ujumbe mshambiliaji wa Simba, Leonel Ateba akimtaka aweke akiba ya maneno na afahamu kwamba soka ni vitendo zaidi na sio maneno.

Kauli hiyo ya Bacca ni baada ya kufanikiwa kumzuia Ateba kutofunga bao katika mchezo wa Jumamosi, Oktoba 19 uliomalizika kwa Yanga kuifunga Simba bao 1-0. Kauli ya Bacca ni baaada ya hivi karibuni Ateba kuwachimba mkwara mabeki wa Simba akiwaambia kuwa lazima awafunge bila kutaka kujua majina yao.

Bacca amesema tambo za Ateba zilimuamsha usingizini na kuongeza umakini zaidi katika mchezo huo na ndio maana kwa kushirikiana na wachezaji wenzake walifanikiwa kumfunga mdomo.

Ameongeza kuwa mchezaji anapaswa kumuheshimu mpinzani wake kwani katika soka hakuna maneno bali ni vitendo zaidi.

“Ninavyohisi alikuwa anajipa motisha, alikuwa anajifariji ili ahakikishe mechi hii anafanya vizuri, lakini nimwambie yupo vizuri ila aweke akiba ya maneno,” amesema Bacca.

Related Articles

Back to top button