TDS Girls, JKT Queens wakutana fainali ya CAF U17

DAR ES SALAAM: TIMU za Tanzania, TDS Girls na JKT Queens zitakutana kwenye mchezo wa fainali ya michuano ya U 17 Girls Integrated Football Tournament (GIFT) utakaochezwa uwanja wa Azam Complex, Chamazi.
Fainali hiyo iliyokuwa imepangwa kufanyika Jumamosi, Januari 18 saa 12:00 jioni na sasa itachezwa saa 1:00 usiku, Azam Complex uliopo Chamazi nje kidogo ya Dar es Salaam.
Taarifa iliyotolewa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) kuwa marekebisho ya muda wa kuanza kwa mechi yalifanywa kuhakikisha timu hizo mbili kutoka Tanzania zimepata muda wa kufanya maandalizi.
Mashindano ya GIFT yanaendelea leo, Ijumaa, Januaria 17 kutafuta mshindi wa tatu kati ya mshindi wa kundi A, Kenya Academy of Sports dhidi ya Boni Consili Girls kucheza saa 18:00 jioni.
Mchezo wa kuwania nafasi ya tano kati ya Kenya Elite Junior Academy dhidi ya Aigle Noir, utacheza saa 9:00 mchana.