Burudani

Ariana Grande ‘atetemeka’ kuteuliwa tuzo za Oscar

MWANAMUZIKI anayetamba na wimbo wa ‘Thank U, Next’, Ariana Grande ameonekana kuwa na hisia kali baada ya kuorodheshwa katika kipengele cha Muigizaji Bora wa Kike katika Tuzo zijazo za Academy.

Ariana katika filamu ya ‘Wicked” amecheza kama Galinda, na wakati wote alionekana kuzidiwa na furaha kiasi kwamba akaamua kuandika katika ukurasa wake wa Instagram akielezea hisia zake na kuwashukuru waliomsaidia kuigiza vyema katika filamu hiyo.

Ariana Grand aliandika: “Nikiinua kichwa changu najikuta nalia huku nikisema asante sana kwa @theacademy kwa utambuzi huu usioelezeka. Siwezi kuacha kulia kwa mshangao!

“Asante tena, kutoka chini ya moyo wangu, kwa uthibitisho huu @theacademy.”
Ariana pia alimpongeza mkurugenzi Jon M. Chu na mwigizaji mwenzake Cynthia Erivo, ambaye ameteuliwa kuwa Muigizaji Bora wa Kike.

Ariana aliongeza: “Asante @jonmchu kwa kuchukua nafasi hii kwangu na kwa kuwa kiongozi mahiri zaidi, binadamu na rafiki mkali zaidi. Ninajivunia sana familia hii na namna nilivyochaguliwa kugombea nafasi hiyo.

“Ninajivunia pia kwa Elphie wangu, dada yangu kipenzi, kipaji chako hakikomi na unastahili kila ua kutoka katika kila bustani.

“Sina maneno mengi, bado najaribu kupumua. lakini asante. Oh Mungu wangu, asante. Universal, Marc, familia yangu, moyo wangu unasema asante.

Filamu ya ‘Wicked’ aliyoshiriki Ariana Grand ikiwa imeongozwa na John M. Chu imepokea jumla ya teuzi 10 za Oscar, jambo lililomfurahisha mkurugenzi Jon na mwanamuziki huyo.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button